Habari za michezo

BAADA YA KUISOMA KMC YA HITIMANA KWA KINA…NABI KAKUNA KICHWA WEEH..KISHA AKASEMA HAYA…

admin March 18, 2022 10:14 am


NJE ya uwanja, tayari Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi amewamaliza wapinzani wake, KMC wenye maskani yao Kinondoni, Dar es Salaam.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana kesho Jumamosi saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara raundi ya 18.

Katika mchezo huo, Yanga itaingia uwanjani ikitaka kuendeleza rekodi yake ya kutopoteza msimu huu kunako ligi huku ikiwa kileleni na pointi 45.

Nabi alisema ataingia uwanjani katika mcheza huo akiwa anaifahamu KMC ambayo imekuwa na tabia ya kukamia kila wanapokutana.

Nabi alisema tayari amekaa na wachezaji wake kufanya nao kikao kwa ajili ya kuwapa tahadhari kwa kuhakikisha wanatumia kila upungufu wa wapinzani ambapo amewaambia ili kuhakikisha wanatumia vema kila nafasi watakayoipata.

Aliongeza kuwa, tayari ameshaona upungufu huo wa wapinzani wao kupitia video za michezo ya mwisho ambayo wamecheza ikiwemo dhidi ya Coastal Union.

“Mimi kila mchezo ulio mbele yangu nitacheza kama fainali, hilo wanalifahamu wachezaji wangu, hiyo ni katika kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu ya msimu huu ya kutopoteza mechi katika kila mchezo.

“Lengo ni tuendelee kukaa kileleni katika msimamo wa ligi, na hilo linawezekana kwetu kutokana na maandalizi ambayo tumeyafanya na hatutaidharau timu yoyote tutakayokutana nayo kwani tunafahamu kila timu inacheza kwa kutupania.

“Tunakwenda kucheza mchezo ujao wa ligi dhidi ya KMC tukiwa tunaifahamu vizuri kwa maana ya mbinu na aina ya uchezaji wao, hivyo nimewaambia vijana wangu kutumia upungufu waliokuwa nao wapinzani kwa lengo la kupata matokeo mazuri,” alisema Nabi.

Itakumbukwa kuwa, timu hizo zilipokutana katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 0-2 ugenini.

AHMED ALLY – KUPONA KWA MKUDE ILIKUWA NI BAHATI MBAYA KWA WAARABU…ALIWAFANYA VIBAYA SANA.. ZIMBWE Jr AKOLEZA CHUMVI KUELEKEA MECHI NA WAIVORY…ATOFAUTIANA NA MABOSI ZAKE SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply