Home Habari za michezo SIMBA WAZIDI KUTIKISA AFRIKA…WAISHUSHA RASMI AL AHLY KWENYE REKODI ZA CAF…YAWA GUMZO...

SIMBA WAZIDI KUTIKISA AFRIKA…WAISHUSHA RASMI AL AHLY KWENYE REKODI ZA CAF…YAWA GUMZO …


Tathimini iliyofanywa kwenye akaunti za Mitandao ya kijamii za Shiriskiho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ imebaini kuwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wanaongoza kutazamwa na Mashabiki wengi zaidi wanapocheza michuano ya kimataifa.

Kwa mujibu wa CAF, Simba imekuwa ikifuatiliwa kupitia Youtube Channel (CAF TV) kulinganisha na timu nyingine kongwe katika Bara la Afrika ikifuatiwa na Al Ahly ya Misri.

CAF ilianza Rasmi kutupia Videio fupi za matukio ya Michezo ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho msimu wa 2020/21 kuanzia hatua ya Makundi hadi Fainali.

Rekodi zinaonyesha pambano lililotazamwa zaidi ni lile la Simba vs Al Ahly la msimu uliopita ambapo Simba ilishinda 1-0, kwani lilitazamwa na mashabiki zaidi ya milioni moja, huku maoni yakiwa zaidi ya 800.

Mchezo ulioshika nafasi ya pili ni Simba na AS Vita uliopigwa Dar es salaam ukitazamwa na mashabiki 597,000 na ule wa ugenini ambayo Simba SC ilishinda bao 1-0 na mpaka sasa mchezo huo umetazamwa na watu 529,000 katika chaneli ya CAF TV.

Michezo mingine iliyotazamwa kwa wingi pia ikiihusisha Simba SC ni Robo Fainali dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini uliyopata watazamaji 177,000 na ule dhidi ya Al Ahly iliyopigwa mjini Cairo-Misri ukitazamwa na watu 169,000.

Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu uliopita kati ya Al Ahly dhidi ya Kaizer Chiefs hadi sasa imetazamwa na watu 153,000, hatua ambayo inaonyesha namna gani Simba SC inavyotisha ndani ya CAF TV.

Msimu huu Simba SC ikishiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika, pambalo lake la kwanza hatua ya Makundi dhidi ya ASEC Mimosas lililopigwa Jijini Dar es salaam Uwanja wa Benjamin Mkapa limetazamwa na watu 183,000, likifuatiwa na Simba SC dhidi ya RS Berkane uliopigwa Jumapili (Machi 13) Jijini Dar es salaam lililopata watazamaji 127,000 hadi sasa.

Mchezo wa ugenini ambapo Simba SC ilipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya RS Berkane, umetamwa na watu 115,000 hadi sasa.

SOMA NA HII  BAADA YA TETESI ZA KUMALIZANA NA YANGA KUZAGAA....DUBE KAIBUKA NA HILI JIPYA...

Hata hivyo Simba SC kuna michezo yake miwili ya msimu uliopita imepata watazamaji wachache ukiwemo mchezo dhidi ya El Merrikh uliochezwa mjini Khartoum-Sudan umetazamwa na watu 56,000 na ule wa USGN ya Niger uliopigwa ugenini mjini Niamey msimu huu ukitazamwa na watu 97,000.

Hadi sasa tafsiri ya kutazamwa huko ni kwamba CAF TV na mitandao yao itajiongezea kipato zaidi siku zijazo kupitia ubora wa na mvuto Simba SC.