kimataifa

WAARABU WA NEWCASTLE WAFUNGUA POCHI KUMTAKA NEYMAR..BARCELONA NA MAN CITY MHHH…

admin March 22, 2022 6:30 pm


MABOSI wa newcastle United wameamua kuonyesha jeuri ya pesa kwa kuamua kujitosa kwenye dili la kuiwania saini ya staa wa PSG na Brazil, Neymar ambaye amekuwa akiwindwa na Manchester City na Barcelona.

Neymar anaonekana kuwa na wakati mgumu kwenye viunga vya PSG na taarifa zinadai ameomba kuondoka mwisho wa msimu huu. Mkataba wake unatakiwa kumalizika 2025.

Hata hivyo, Newcastle United haipewi nafasi kubwa ya kuipata huduma ya fundi huyo kama ilivyo Manchester City na Barcelona.

Kuna uwezekano mkubwa Neymar akajiunga na Barcelona kwa sababu mabosi wa timu hiyo tayari wameonyesha nia ya kutaka kumrudisha tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi. Msimu huu Neymar amecheza mechi 21 za michuano yote, amefunga mabao matano na asisti tano.

LAANA YA KUITUKANA SIMBA YAZIDI KUMTAFUNA AUSSEMS….AZIDI KUPATA MATOKEO MABOVU KENYA… DANTE – MAYELE ANGENIUA JAMANI…MFUPA ULIKUWA UNAWAKA MOTO…AFUNGUKA ALICHOKIONA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply