Habari za michezo

RASMI…INJINIA HERSI AFUNGUKA ISHU YA KUMSAJILI AZIZ KI YANGA…ADAI YANGA HAIKURUPUKI…

admin March 27, 2022 1:34 pm


BAADA ya kuibuka kwa tetesi kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye mpango wa kumsajili nyota wa Asec Mimosas ya Ivory Coast, Stephane Aziz Ki, Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Eng. Hersi Said ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM ambao ni wadhamini wa klabu hiyo, amefunguka ukweli wa jambo hilo.

Hersi aliweka wazi na kukubali kuwa ni kweli wamemuona nyota huyo na kukubali uwezo wake, ila ni ngumu kusema kuwa watamsajili kwa sasa kwa kuwa hawataki kukurupuka kwenye sekta hiyo na nguvu kubwa kwa sasa wamewekeza kwenye kulisaka taji la ligi kuu.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari juzi, Injinia Hersi alisema: “Ni kweli tuna idadi kubwa ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwisho wa msimu. Hatukurupuki kuongeza mikataba, malengo yetu kwa sasa ni kombe la ligi kuu ili tupate nafasi ya kuiwakilisha nchi.

BAADA YA KUKIANGALIA KIKOSI CHA SIMBA KINAVYOCHEZA..CHUJI AMEGUNA ..KISHA AKASEMA HAYA… BREAKING….MASTAA SIMBA WAONDOLEWA TAIFA STARS…SABABU HIZI HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply