Habari za michezo

WAKATI RASHFORD AKIONEKANA ‘KITUKO’ MAN UTD…ARTETA NA ARSENAL YAKE WANAMTOLEA ‘UDENDA’ ETI..

admin March 28, 2022 6:33 pm


ARSENAL itapambana kumsajili fowadi wa Manchester United, Marcus Rashford katika kipindi kijacho cha usajili wa majira ya joto, kwa mujibu wa taarifa.

Kikosi hicho cha Mikel Arteta kitakuwa na upungufu wa mastraika mwishoni mwa msimu kwa kuwa Alexandre Lacazette na Eddie Nketiah wote wanamaliza mikataba yao ifikapo Juni.

Na mastraika hao wawili wamefunga bao moja tu la ligi kwa jumla mwaka huu.

Pia Arsenal ilimruhusu nahodha wao wa zamani, Pierre-Emerick Aubameyang kujiunga na Barcelona, Januari.

Hii imewafanya wawe na shauku kubwa ya kupata straika makini, na Arsenal wanamuona Rashford kama straika bora, kwa mujibu wa The Mirror, Rashford amekosa namba kwa miezi ya hivi karibuni pale Old Trafford.

KOCHA MSOMALI WA AZAM FC APIGA MKWARA YANGA..AFUNGUKA ‘ATAKAVYOWATOBOLEA MTUMBWI’… DAH…DILUNGA NDIO BASI TENA SIMBA…PABLO KAONA ISIWE TABU…KAMUONDOA JUMLA JUMLA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply