Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA USGN…PABLO KAONA ISIWE TABU…KAANIKA HALI JINSI ILIVYO…WACHEZAJI WAHUSIKA…

KUELEKEA MECHI NA USGN…PABLO KAONA ISIWE TABU…KAANIKA HALI JINSI ILIVYO…WACHEZAJI WAHUSIKA…


Kocha Mkuu wa Simba SC Franco Pablo Martin, amesema hakuna njia ya mkato kwa kikosi chake zaidi ya kusaka ushindi katika mchezo wa ‘Kundi D’ Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya US Gendarmerieya Niger.

Simba SC itakua mwenyeji Jumapili (April 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku mchezo huo ukitarajiwa kuanza saa moja usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Kocha Pablo amesema anatambua umuhimu wa mchezo huo, na ndio maana maandalizi yake ameyaelekeza katika mpango wa kushinda mchezo huo, ambao umebeba hatma ya kikosi chake kutinga Robo Fainali.

“Ninafahamu umuhimu wa mchezo wetu dhidi ya USGN, nimejiandaa vizuri ili kufanikisha lengo la ushindi ambalo litatuvusha kutoka hatua ya Makundi na kwenda Robo Fainali.”

“Ninatarajia mchezo utakua mgumu sana, tena sana, lakini wachezaji wangu watatakiwa kupambana kwa moyo wao wote ili kufanikisha mpango wa ushindi tuliojiwekea,”

“Ninawaomba Mashabiki wetu wafike Uwanjani, kuja kutupa nguvu ili kufanikisha azma yetu ya kupata ushindi katika Uwanja wetu wa nyumbani.” amesema Pablo

Simba SC itamkosa Hassan Dilunga ambaye ni majeruhi kwa sasa, huku Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Senegal Pape Ousman Sakho akipata majeraha madogo akiwa mazoezini jana Jumatatu (Machi 28).

Simba SC iliyo inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi D ikiwa na alama 07 sawa na RS Berkane ya Morocco, huku ASEC Mimosas ya Ivory Coast ikiongoza kwa alama 09 na US Gendarmerieya Niger inaburuza mkia ikiwa na alama 05.

SOMA NA HII  UMBRO YAWEKA MKONO NDONDO CUP