Habari za michezo
BAADA YA KUFUNGWA NA SENEGAL..MISRI WAONA ISIWE TABU..WAKIMBILIA KUFUNGUA KESI FIFA…
Chama cha soka nchini Misri kitawasilisha malalamiko yake kwa Shirikisho la Soka Ulimwenguni, FIFA, kulalamikia vitendo vya mashabiki wa Senegal kuwasumbua kwa tochi zenye mwanga mkali wachezaji wake wakati wa mchezo wa marudiano kufuzu kombe la Dunia.
FA ya Misri inadai vitendo hivyo vimechangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kupoteza kwa mikwaju ya penati katika mchezo huo.
Kuna matumaini huenda Senegal ikaadhibiwa kwa kutozwa faini kwa vitendo hivyo vya mashabiki wake.

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.