Habar za Usajili Simba

KULEKEA MECHI YA JUMAPILI DHIDI YA USGN..PABLO AIBUKA NA HILI TENA…AJIPA JUKUMU KWA MASHABIKI…

admin March 30, 2022 3:26 pm


Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba Pablo Franco ameweka wazi kuwa wanahitaji kupata ushindi katika mchezo wao wa jumapili wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya US Gandarmerie ili kuwapa furaha mashabiki wao.

Kauli hiyo imesemwa na Pablo kuwa anaamini mashabiki watajitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa hiyo itakuwa jambo zuri kushinda ili kusherehekea kwa pamoja.

“Tunajua tunahitaji kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu, naamini watajitokeza kwa wingi Jumapili hivyo ni jukumu letu kuhakikisha wanafurahi,” amesema Pablo” amesema Pablo.

Vile vile kocha Pablo ambae ni raia wa Hispania ameongeza kuwa lengo la kwanza ni kuhakikisha wanashinda katika mchezo huo ambao ni kama fainali kwao , lakini pia kuonyesha kandanda safi la kuvutia mashabiki watakaojitokeza.

Kikosi cha Simba kilingia kambini tangu juzi mchana na kuanza rasmi kufanya mazoezi jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo.

BAADA YA KUFUNGWA NA SENEGAL..MISRI WAONA ISIWE TABU..WAKIMBILIA KUFUNGUA KESI FIFA… RASMI…’FEI TOTO’ APIGWA ‘STOP’ KUCHEZA MPIRA…MADAKTARI WAMPA ONYO..ASIPOZINGATIA IMEKULA KWAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply