Home Habari za michezo AHMED ALLY AIBUA KAMPENI MPYA SIMBA…WAPANIA KUMALIZA KAZI BENIN…WATAKA REKODI HII MPYA…

AHMED ALLY AIBUA KAMPENI MPYA SIMBA…WAPANIA KUMALIZA KAZI BENIN…WATAKA REKODI HII MPYA…


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu ya Simba SC Ahmed Ally amesema lengo kuu la kikosi chao kuelekea Benin ni kuendeleza mapambano katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Kikosi cha Simba SC kimeondoka Dar es salaam mapema jana Ijumaa (Machi 18) majira ya Alfajiri kuelekea mjini Cotonou-Benin kikipitia mjini Adis Ababa-Ethiopita.

Ahmed alizungumza na waandishi wa habari dakika chache kabla ya kikosi cha Simba SC kuanza safari ya Benin, ambapo alisema wanatambua umuhimu wa mchezo dhidi ya ASEC Mimosas hivyo Benchi la Ufundi na Wachezaji kwa ujumla wamejiandaa kikamilifu ili kufanikisha wanapata matokeo mazuri katika Uwanja wa Ugenini.

“Tunakwenda kupambana na ASEC Mimosas tukiwa na Kampeni moja kubwa, kwamba tunataka kufuzu tukiwa ugenini, mara kadhaa tumeshafuzu kucheza hatua ya Robo Fainali katika michuano ya Afrika, lakini mara zote imekua tukifanya hivyo tukiwa nyumbani Tanzania,”

“Tunafuzu vipi? ni kwa kumfunga ASEC Mimosas katika Uwanja wake wa nyumbani, tunaamini hilo linawezekana na ndio maana tupo tayari kwenda kupambana vilivyo ugenini,”

“Tukimgunga ASEC Mimosas tutafikisha alama 10 na tayari tutakua tumeshafuzu kwa hatua ya Robo Fainali, hivyo mchezo wetu wa mwisho tutakaocheza hapa Dar es salaam dhidi ya USGN tutakuja kucheza kwa kuwaburudisha mashabiki wetu.” Alisema Ahmed Ally kabla ya kuanza safari ya kuelekea Benin

Simba SC inaongoza msimamo wa Kundi D ikiwa na alama 07 baada ya kuifunga RS Berkane Jumapili (Machi 13), Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam, huku ASEC Mimosas ikiwa nafasi ya pili kwa ufikisha alama 06.

RS Berkane imefungana kwa alama na ASEC Mimosas lakini ipo nafasi ya tatu, huku USGN ikiburuza mkia wa Kundi D kwa kufikisha alama 04.

SOMA NA HII  MCHAWI WA SIMBA APATIKANA