Home Habari za michezo CHAMA AZINGUA MAZOEZINI SIMBA…AINGIA KWENYE ‘HISTORIA MBAYA’..ASHINDWA KUPIGA PENATI…

CHAMA AZINGUA MAZOEZINI SIMBA…AINGIA KWENYE ‘HISTORIA MBAYA’..ASHINDWA KUPIGA PENATI…


KAMA unadhani mzimu wa kukosa penalti kwa Simba unaisumbua kwenye mechi za mashindano tu, pole yako kwani hata mazoezini tatizo hilo linaendela kuwatibua mastaa wa timu hiyo akiwamo Clatous Chama.

Chama aliyefunga mkwaju wa penalti katika Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji wakati timu hiyo ikishinda mabao 2-0, wengi waliamini mambo yameanza kunyoosha kwa Simba, lakini juzi buana kiungo huyo fundi kutoka Zambia alikosa penalti katika mechi ya kirafiki ya mazoezini dhidi ya Cambiaso.

Simba ilivaana na Cambiaso katika mechi iliyopigwa Uwanja Mo Simba Arena na kushinda mabao 2-1 huku Chama alikosa penalti dakika ya 68 na Simon Msuva akikosa 44.

Penalti ya Simba ilitokana Bernard Morrison kuwapangua mabeki aliyomuangusha ndani ya 18 na aliyokosa Msuva ilitokana na yeye mwenyewe kuangusha ndani ya 18 na walinzi wa Wanamsimbazi, lakini ndiye mfungaji wa bao.

Mechi hiyo, ilikuwa kipimo kizuri kwa Simba, kutokana na ubora wa Cambiaso iliyo chini ya kocha Mecky Maxime, kupambana kuanzia dakika ya kwanza hadi ya 78 mchezo ulipomalizika.

Ukiachana na hilo, kukosa penalti kwa Chama katika mechi ya kirafiki ni muendelezo wa kile kinachotokea mechi za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Africa (CAF).

Hilo linathibitishwa kutokana na takwimu zilizotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Simba licha ya kuongoza kupata penalti nyingi imepata chache.

Nahodha wa kikosi hicho, John Bocco alikosa dhidi ya Biashara United, Erasto Nyoni dhidi ya Ruvu Shooting, Larry Bwalya dhidi ya Azam FC,Chama kapata dhidi ya Dodoma Jiji,Bwalya kapata dhidi ya Polisi Tanzania, Meddie Kagere kapata dhidi ya Prisons na kakosa dhidi ya Biashara United na Cris Mugalu kakosa na Mbeya City.

Katika michuano ya CAF beki Shomary Kapombe alipata dhidi ya Asec Mimosas, Simba ikishinda mabao 3-1, huku Morrison akikosa dhidi ya Red Arrows akifunga mawili kati ya 3-0 na kutoa asiti ya bao alilofunga Kagere.

Kutokana na mwenendo wa kukosa penalti, beki wa zamani wa timu hiyo, Boniface Pawassa alisema ili mradi kuna changamoto hiyo, kocha Pablo Franco anapaswa kuwapa mazoezi zaidi ya kupiga, ili wakicheza mechi wajiamini zaidi.

SOMA NA HII  FIFA WAIBUKA NA HILI JIPYA SAKATA LA MABILIONI YA MSUVA KUTOKA KWA WAARABU....

“Hilo siyo Simba tu, wakati mwingine inakuwa ni upepo mbaya, lakini lisiwatishe wanapaswa kufanya mazoezi makali yatakayowafanya wajiamini zaidi,” alisema.

Kauli yake iliungwa mkono na mkongwe mwingine, Emmanuel Gabriel aliyesema ilimradi tatizo la kupiga penalti linawaandama inafaa kufanyiwa mazoezi mara kwa mara hadi watakapoliondoa.

“Hakuna mchawi zaidi ya mazoezi, kitu ukikifanya sana ndivyo unavyokuwa bora, hata kufunga hakuji kwa bahati mbaya lazima mazoezi ya kufunga yafanyike, hata wachezaji wenyewe wapate muda wa ziada wenyewe kwa wenyewe wawe wanafanya mazoezi hayo,” alisema.