Home Habari za michezo KAPOMBE AZIDI KUTAKATA SIMBA…KUSHINDANA NA SAKHO TUZO YA MCHEZAJI BORA…

KAPOMBE AZIDI KUTAKATA SIMBA…KUSHINDANA NA SAKHO TUZO YA MCHEZAJI BORA…


Beki wa kulia Shomari Salum Kapombe ametajwa tena kwenye orodha wa wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Machi Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC.

Kapombe alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo mwezi uliopita akiwashinda Kiungo Mshambuliaji kutoka Malawi Peter Banda na Beki kutoka DR Congo Henock Inonga.

Kwa Mwezi huu Machi Kampombe anashindanishwa na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Malawi na Pape Sakho (Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Senegal).

Simba SC imetoa orodha hiyo leo Jumatano (Machi 23), ambapo mashabiki wa klabu hiyo wataanza kupiga kura na baadae mshindi atatangazwa kupitia kurasa za Mitandao ya Kijamii za Mabingwa hao wa Tanzania Bara. Mbali na Kapombe kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Simba SC mwezi Februari, Pape Ousman Sakho alitangazwa kuwa mshindi wa mwezi Januari, huku Kiungo Jonas Mkude akiibuka kidedea mwezi Desemba 2021.

SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KUWAIGA KILA JAMBO....SIMBA WAJA NA HILI JIPYA KUHUSU 'KISPIKA MTAANI'....