Home Habari za michezo KUHUSU KUFUNGA NA KUSHANGILIA KWA KUTETEMA…MAYELE KWA MARA YA KWANZA KASEMA HAYA…

KUHUSU KUFUNGA NA KUSHANGILIA KWA KUTETEMA…MAYELE KWA MARA YA KWANZA KASEMA HAYA…


FISTON Mayele mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kuweza kufunga mabao 10 ndani ya ligi ni kutimiza majukumu yake pamoja na kufanya kile anachokifanya mazoezini.

Msimu wa 2021/22 Mayele amecheza mechi 18 na kufunga mabao 10 kati ya 31 ambayo yamefungwa na timu hiyo na ametoa pasi 3 za mabao.

Mayele amesema kuwa anafunga kila anapopata nafasi ya kufunga kwa kuwa ni kazi yake kila anapokuwa uwanjani.

β€œNinafunga kwa sababu ni majukumu yangu pia  ninajua kwamba ili timu iweze kushinda inahitaji kuweza kufunga jambo ambalo linafanya ninakuwa bora.

β€œKitu kingine ni kwamba mazoezi ambayo ninafanya ni kitu muhimu pia kwa kuwa yananifanya ninakuwa imara na ninapenda kuona inakuwa hivyo kila mechi,” amesema Mayele.

SOMA NA HII  MWAIKIMBA ASIMULIA ALIVYOLAMBA MILIONI 58 ZA M-BET TANZANIA KIULAINII...KITAMBULISHO CHA NIDA KILIMCHELEWESHA...