Home news SSETUBA: HUYU CHAMA JAMANI SIYO MTU WA KAWAIDA…AFUNGUKA ALIVYOMTESA KWA CHENGA MATATA…

SSETUBA: HUYU CHAMA JAMANI SIYO MTU WA KAWAIDA…AFUNGUKA ALIVYOMTESA KWA CHENGA MATATA…


Malinda Lango wa Biashara United Mara James Ssetuba amekiri uwezo mkubwa wa nyota wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Clatous Chama na Pape Ousmane Sakho ulichangia kwa kiasi kikubwa kuwazamisha katika mchezo wa Mzunguuko wa 16 wa Ligi Kuu juzi Ijumaa (Macho 04).

Simba SC ilikua mwenyeji wa mchezo huo uliounguruma Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam, huku ikiichabanga Biashara United Mara mabao 3-0.

Mlinda Lango huyo aliyeonekana kujutia hasa baada ya kufungwa bao la tatu amesema: “Sakho na Chama sio wachezaji wa kawaida, wanajua sana, na wakiwa katika eneo lao sio wa kuwachezea na hata aina ya mabao ambayo wamenifunga ni ya kiufundi,”

“Ukiangalia mabeki wangu walipoteana pale, nikabakia mimi langoni alafu kwa akili za Chama aliwachambua na kunifunga bao la kiufundi sana.”

Mabao ya Simba SC katika mchezo huo yalipachikwa wavuni na Viungo Clatous Chotta Chama, Mzamiru Yassin na Pappe Ousmane Sakho katika kipindi cha kwanza.

SOMA NA HII  YANGA HAWATANII AISEE....WAMWAMGIA MAMILIONI YA PESA BEKI MGANDA...MICHO NA AUCHO WAHUSISHWA...