Home news ‘UCHAWI’ WA CHAMA WAZIDI KUMKOLEA PABLO…KAONA LIWALO NA LIWE…AAMUA KUMPA KITENGO KIPYA...

‘UCHAWI’ WA CHAMA WAZIDI KUMKOLEA PABLO…KAONA LIWALO NA LIWE…AAMUA KUMPA KITENGO KIPYA SIMBA…


Kocha Mkuu wa Simba SC Franco Pablo Martin amemkabidhi jukumu la kupiga Penati Kiungo kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama, baada ya kufanya kazi hiyo kwa usahihi kwenye mchezo wa Mzunguuko wa 17 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Chama aliifungia Simba SC bao la kuongoza kwa mkwaju wa Penati katika mchezo huo, uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam Jumatatu (Machi 07).

Kocha Pablo amesema asilimia kubwa ya wachezaji wake wameingia uwoga wa kubeba jukumu la kupiga Penati, hivyo ameona kuna haja ya Chama kuendelea na jukumu hilo, kama atakuwa sehemu ya kikosi.

“Ukiangalia wengi wanaonekana kuogopa, nafikiri inatokana na hii baadhi kuzipoteza karibuni.”

“Angalia alivyojiamini (Chama). Nafikiri ni vyema kumpa mtu jukumu hili ambaye anaonyesha kujiamini na kama atakuwepo ndani ya uwanja chaguo la kwanza litakuwa kwake,” amesema Kocha Pablo Franco.

Bao lingine la Simba SC katika mchezo huo lilikwamishwa wavuni na Mshambuliaji kutoka nchini Rwanda Meddie Kagere kwa kichwa, akimalizia mpira wa Krosi uliopigwa na Kiungo Mshambuliaji kutoka Malawi Peter Banda.

SOMA NA HII  SIMBA WAZINDUA KAMPENI YA KUWAMALIZA WASAUZI KWA MKAPA...MZEE DALALI AMWAGA 'ASALI'....