Home Habari za michezo WAKATI JAHAZI LA MAN UTD LIKIWA HALIELEWEKI…RIO FERDINAND ATABIRI HAYA KUHUSU RONALDO…

WAKATI JAHAZI LA MAN UTD LIKIWA HALIELEWEKI…RIO FERDINAND ATABIRI HAYA KUHUSU RONALDO…


MCHEZAJI wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, amesema haoni mchezaji mwenzake wa zamani, Cristiano Ronaldo akiondoka kwenye klabu hiyo kipindi cha majira ya joto hata kama watashindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ferdinand amecheza pamoja na Ronaldo pale Man United kuanzia mwaka 2003 hadi 2009, ambapo walikuwa chini ya kocha Sir Alex Ferguson huku wakifanikiwa kuchukua ubingwa wa Ulaya, Ligi Kuu mara tatu, FA mara moja na Kombe la Ligi mara mbili.

Ronaldo amejiunga na klabu ya Man United kipindi cha majira ya joto mwaka 2021, lakini tangu amejiunga kumekuwa na tetesi za kuwa anaweza kuondoa ikiwa tu, timu hiyo itashindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Sioni kama ataondoka, nataka kuwa mkweli, hata kama Man United wakishindwa kuingia kwenye nne bora,” alisema Ferdinand.

“Nafikiri Ronaldo anapaswa kushugulika na Man Utd kwa mwaka mwingine. Ndio anataka kushindana, anayo hiyo hamasa ya kutaka kushinda mataji, alishazoea kufanya hivyo, amezoea kushinda tu.

“Lakini mara zote haiwezi kuwa hivyo, amekuwa na misimu mizuri karibia miaka yake yote.”

SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI HUYU BYE BYE YANGA...PRINCE DUBE KUCHUKUA NAFASI YAKE