Home Habari za michezo BAADA YA ‘SPIDI’ YA SIMBA KUMPA ‘PRESHA YA TUMBO’… NABI KAONA ISIWE...

BAADA YA ‘SPIDI’ YA SIMBA KUMPA ‘PRESHA YA TUMBO’… NABI KAONA ISIWE TABU..KAFANYA UAMUZI HUU CHAP…


KUTOKANA na presha wanayoipata kutoka kwa wapinzani wao Simba SC katika kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amewaambia wachezaji wake kwamba, wanapaswa kuipambania timu katika mechi kumi zilizosalia, kwani mwisho wa msimu atafanya uamuzi mgumu.

Nabi ametoa maagizo hayo ikiwa Yanga inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na alama 48 baada ya kucheza mechi 18. Imesaliwa na mechi kumi zenye jumla ya pointi 30 kukamilisha msimu huu.

Licha ya Yanga kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 11 dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na mchezo mmoja mkononi, lakini haina uhakika wa kuwa mabingwa kwani ikiteleza kidogo tu, hawana chao. Ndani ya kikosi cha Yanga, kuna wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwisho wa msimu huu, hivyo Nabi amewataka wachezaji wote wakiwemo wanaomaliza mikataba yao, kuonesha viwango vikubwa kipindi hiki kwani atakayezembea, hatakuwa naye msimu ujao.

Miongoni  mwa wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu ni Saidi Ntibazonkiza, Yassin Mustapha, Bakari Mwamnyeto, Kibwana Shomari, Zawadi Mauya, Farid Mussa, Deus Kaseke na Paul Godfrey.

Chanzo kutoka Yanga, kimefunguka kuwa: “Unajua sasa hivi viongozi hawataki kuzungumzia kabisa masuala ya mikataba ya wachezaji ambayo inaisha mwishoni mwa msimu huu. “Sababu kubwa ambayo inafanya wao wasizungumziehilo ni kutaka wabebe ubingwa wa ligi kuu msimu huu na wapo makini sana kwani waliwaambia wachezaji na benchi la ufundi juu ya jambo hilo.

 “Walishakaa kikao na wachezaji ambao wanamaliza mikataba yao na kuwaeleza kila mmoja kwa juhudi zake ndizo zitamfanya kuongezewa mkataba. “Lakini pia hata wale ambao bado wana mikataba, wameambiwa waendelee kupambana kwani atakayezingua, msimu ujao hatakuwa sehemu ya kikosi. “Hivyo suala la wachezaji kuwaza mikataba kwa sasa halipo, wanachofikiria zaidi ni ubingwa wa ligi.”

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Ufundi ya Yanga, Dominick Albinus, aliliambia Spoti Xtra kwamba: “Kwanza kabla ya watu kujua mikataba ya wachezaji, sisi ndio tunajua mkataba wa nani unamalizika kwa muda gani. 

SOMA NA HII  YANGA WACHIMBA MKWARA MZITO LIGI KUU BARA

“Naomba niwahakikishie Wanayanga wote kuwa hakuna mchezaji yeyote muhimu atakayeondoka kwenye kikosi chetu, zaidi tuna mpango wa kuimarisha hawa waliopo na sio kubomoa. “Kwa hiyo wachezaji wote waliopo na wanaohitajika na kocha basi wataendelea kubaki kwenye kikosi na hakuna hata mmoja atakayeondoka.”