Habari za michezo

DAKIKA 90 ZA YANGA vs GEITA JANA HAZIKUWA RAHISI AISEE….ILIBAKI ‘KIDUNCHU’ TU MENGINE YATOKEE…

admin April 11, 2022 7:32 am


Young Africans wametinga Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Azam Sport Federation (ASFC) baada ya kuitoa Geita Gold kwa  mabao 7-6 kwa Mkwaju wa Penalti baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 kwa kufungana bao 1-1 mchezo uliopigwa jana uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Geita walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 86 likifungwa na Offen Chikola na Shaban Djuma aliisawazishia Yanga dakika ya 90 kwa Mkwaju wa Penalti baada ya beki wa Geita kuunawa Mpira.

Mpaka dakika 90 zinamalizika timu hizo zilitoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 na ikapelekea kwenda kwenye Mkwaju wa Penalti.

Kwa Matokeo Yanga wametinga Nusu Fainali na watakutana mshindi kati ya Simba au Pamba kutoka jijini Mwanza mchezo utakaopigwa kati ya Arusha au Mwanza.

KUELEKEA MECHI NA WASAUZI..HII HAPA SABABU KWA NINI MORRISON ANAWEZA KUIBEBA SIMBA… SERIKALI SAUZI WAZIDI KUMKAZIA MORRISON…BARBARA AANIKA ALIVYOJIBIWA A-Z…AGUSIA KOSA LAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply