Habari za michezo

KUHUSU ISHU YA MABADILIKO YA RATIBA MECHI YA YANGA vs SIMBA…BODI YA LIGI WAJA NA KAULI HII….

admin April 16, 2022 12:25 pm


Bodi ya Ligi Kuu ya NBC imethibitisha kuwa hadi sasa haijapokea maombi yoyote ya kusogezwa mbele kwa mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga ambao umepangwa kuchezwa April 30,2022.

Akizungumza na East Africa Radio kwenye kipindi cha Michezo cha Kipenga kinachoruka kila siku kuanzia saa 2 hadi saa 3 usiku, Afisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda amesema mechi kati ya Simba na Yanga itachezwa katika tarehe na siku ilyopangwa awali.

”Hadi sasa hatujapokea maombi yoyote ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo, hivyo maandalizi yanaendelea kama kawaida na kila kitu kinakwenda kama kilivypangwa”Alisema Boimanda.

Ufafanuzi huo unakuja siku chache zilizopita kufuatia uvumi uliosambaa mitandaoni kuwa huenda Simba ingeomba kusogezwa mbele kwa mchezo huo kutokana na kuwa na mfululizo wa mechi za kimataifa dhidi ya Orland Pirates mnamo tarehe 14 na 24 hatua ya robo fainali.

WAKATI MASHABIKI WAKIMFURAHIA …NABI KAONA ISIWE TABU….KAAMUA KUMPA MAKAVU LIVE MAYELE… MAJANGA YAZIDI KUMKUTA CHICO USHINDI ….YANGA WAMWEKEA TUMAINI LA KUIKABILI SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply