Aziz Ki Yanga
Yanga SC

RUKSA YA AL-ITTIHAD: Aziz Ki Atua Yanga Kwa Bilioni 1.2? Kamwe Afunguka!

Vardo August 13, 2026 1:40 pm

Wakati masaa yakizidi kuyoyoma kuelekea kufungwa kwa dirisha la usajili, mashabiki wa Yanga SC wameendelea kukaa kwenye viti vya moto kufuatia tetesi zinazozidi kushika kasi kuhusu kurejea kwa kiungo mshambuliaji nyota, Stephane Aziz Ki.

Hata hivyo, uongozi wa Mabingwa hao wa Soka Tanzania Bara umeamua kubaki kimya, huku Msemaji wa Klabu hiyo, Ali Kamwe, akibainisha kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Rais wa Klabu, Hersi Said.

Ali Kamwe: “Kuna Jambo Linaenda Kufanyika”

Akizungumzia uvumi huo, Ali Kamwe amekiri kusikia taarifa hizo lakini akasisitiza kuwa bado hajapewa taarifa rasmi kuhusu kukamilika kwa dili la Aziz Ki.

Hata hivyo, Kamwe alidokeza kuwa Rais Hersi Said alifanya mazungumzo ya kina na Kocha Mkuu, Manqoba Mngqithi, mara baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba SC kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, kwa lengo la kubaini maeneo yanayohitaji marekebisho ya haraka.

“Kuhusu Aziz Ki nimesikia na sijaambiwa lolote, ila Rais Hersi ameniambia kuna kitu kimoja wanaenda kuboresha. Baada ya ushindi wetu dhidi ya Simba aliongea na kocha na kuona ni sehemu gani ya kuboresha. Tusubiri hizi siku mbili tutaona kama kuna jambo linaenda kufanyika,” alisema Kamwe.


Ofa ya Bilioni 1.2 na Safari ya Zanzibar

Kauli ya Kamwe inakuja wakati taarifa za ndani zikidai kuwa Aziz Ki tayari amepewa ruhusa na klabu yake ya Al-Ittihad ya Libya kuendelea na mazungumzo binafsi na Yanga.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Yanga imeweka mezani ofa nono ya Dola 450,000 (zaidi ya Shilingi bilioni 1.2 za Kitanzania) ili kunasa saini ya kiungo huyo aliyekuwa nguzo kuu ya mafanikio ya timu hiyo msimu uliopita.

Inaarifiwa kuwa mchezaji huyo tayari amepewa taa ya kijani kusafiri kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kumalizana na viongozi wa Yanga na kusaini mkataba mpya wa kuitumikia klabu hiyo.

Meridian Leprechaun Wish Yaleta Ladha Ya Kipekee Kwenye Michezo Ya Kasino Ahmed Ally Afunguka Baada ya Kipigo cha Yanga Ngao ya Jamii: “Safari Bado Ndefu”