Israel Mwenda Yanga
Yanga SC

Sakata la Israel Mwenda Yanga Chukua Sura Mpya, Akimbilia SPATA

Vardo September 30, 2026 11:34 am

Sakata la beki wa kulia wa Yanga SC, Israel Mwenda, limeingia katika sura mpya na kuibua mjadala mzito kwenye ulimwengu wa soka nchini baada ya mchezaji huyo kufikisha malalamiko yake kwenye Chama cha Wachezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania (SPATA).

Mwenda amechukua hatua hiyo akiomba msaada wa kisheria na utatuzi wa changamoto zinazomzuia kupata mazingira rafiki ya kuendelea na majukumu yake ndani ya kikosi hicho cha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

SPATA YAthibitisha Kupokea Shauri la Mwenda

Beki huyo amefikisha suala hilo SPATA akitaka chama hicho kinachoongozwa na wachezaji wa zamani kuingilia kati ili kumaliza kile kinachodaiwa kuwa ni mgogoro kati yake na viongozi au benchi la ufundi la Yanga, lengo likiwa ni kurejea uwanjani.

Mwenyekiti wa SPATA, Mussa Kisoki, amethibitisha kupokea malalamiko ya beki huyo na kubainisha kuwa wako tayari kulifanyia kazi baada ya kusikiliza pande zote mbili.

“SPATA ndiyo Chama cha Wachezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania, hivyo kama kuna kitu chochote kinachowahusu ni lazima sisi tujue kwa sababu kanuni inaturuhusu. Kuhusu suala hilo naomba utupe muda na tutalifanyia ufafanuzi,” amesema Kisoki.

Chanzo cha Israel Mwenda Kutengwa Yanga SC

Kuingia kwa SPATA katika sakata hili kunafungua ukurasa mpya kwa Mwenda, ambaye kwa sasa hayupo kikosini licha ya kuwa bado ana mkataba halali na Wananchi. Hali hii imeendelea kuzua maswali mengi miongoni mwa mashabiki kuhusu hatima yake tangu kuanza kwa msimu wa 2026/27.

Ingawa alianza msimu akiwa sehemu ya mipango ya timu, hali ilibadilika ghafla na beki huyo kupoteza namba katika benchi la ufundi.

Inaarifiwa kuwa upepo ulianza kubadilika kufuatia mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya watani wa jadi, Simba SC, uliopigwa Mei 3, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na kumalizika kwa sare ya 2-2. Katika mchezo huo, makosa ya kidefensi yaliyopelekea mabao ya Simba yalihusishwa na Mwenda, hatua iliyoibua hisia tofauti ingawa viongozi wa Yanga walikanusha madai ya mchezaji huyo kufanya makosa kwa makusudi.

Hivi sasa, macho na masikio ya wadau wa soka la Bongo yameelekezwa SPATA kuona ni hatua gani zitachukuliwa kuokoa kipaji na hatima ya mchezaji huyo ndani ya Yanga.

Wiki Mbili Za Matukio Ya Kasino Kupitia Cash Storm