Habari za michezo

BAADA YA KUTAMBULISHWA RASMI LEO…KOCHA MPYA MAN UNITED KAFUNGUKA HAYA…

admin April 21, 2022 2:51 pm


Klabu ya soka ya Manchester United imemtambulisha kocha wa sasa wa Ajax ya nchini Uholanzi Erik Ten Haag kama kocha wao mkuu kwa mkataba wa miaka 3 ukiwa na kipengele cha nyongeza ya mwaka mmoja.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 amewavutia mabosi wa Man United kutokana na kazi yake nchini Uholanzi akiwa na klabu ya Ajax ambao amefanya nao vizuri katika ligi ya ndani lakini pia Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Ten Haag baada ya kutambulishwa amesema:

“Ni heshima kubwa kuchaguliwa kuwa kocha wa Manchester United na najisikia hamasa sana kwa changamoto hii mpya, naijua historia ya klabu hii kubwa pamoja na ari ya mashabiki wake na nimejipanga thabiti kutengeneza timu ya ushindani yenye kuleta mafanikio kwa klabu hii.”

Naye Mkurugenzi wa Michezo wa Manchester United John Murtough ameongeza kwa kusema:

“Kwa kipindi cha miaka minne iliyopita ndani ya kikosi cha Ajax Erik amethibitisha kuwa yeye ni moja ya makocha bora zaidi duniani, akisifiwa kwa falsafa yake ya kushambulia, mpira wa kuvutia na kuwekeza katika vijana.

Kwa sasa klabu ya Manchester United ipo katika nafasi ya sita ya msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza ikiwa na jumla ya alama 54 katika michezo 33 huku ikiwa nyuma ya Arsenal ambayo ipo nafasi ya 5 ikiwa na jumla ya alama 57 katika michezo 32.

KUELEKEA MCHEZO WA PILI SAUZI…BARBARA KAONA ISIWE TABU..KATANGULIA YEYE MWENYEWE…KAFUNGUKA HAYA.. WAKATI SIMBA WAKIWA NA HOFU KUHUSU SAFARI YA AFRIKA KUSINI..SERIKALI WAIBUKA NA TAMKO HILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply