Habari za michezo

WAKATI YANGA WAKIUUMA ANA NAMUNGO….LUSAJO ATAENDELEA KULA MKATE MKAVU LEO…?

admin April 23, 2022 11:01 am


NYOTA wa Namungo, Relliats Lusajo leo anafikisha siku ya 62 bila kufunga bao ndani ya mechi za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.

Nyota huyo mzawa alianza kwa kasi matata na aliweza kuwa namba moja kwa muda kwa watupiaji wa ligi alipofikisha mabao 10 kibindoni.

Mara ya mwisho Lusajo kufunga ilikuwa ni Februari 21,2022 Uwanja wa Ilulu mbele ya Mbeya City ambapo alifunga bao lake la 10 kwenye ligi.

Leo wanatarajiwa kumenyana na Yanga ambao ni vinara wa ligi kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

Ni mabao 11 anayo kinara wa utupiaji ndani ya ligi ambaye ni Fiston Mayele na ana pasi tatu za mabao.

YANGA vs NAMUNGO…UGUMU WA MECHI UKO HAPA…NNJE YA UWANJA VITA NI MANARA NA JULIO… LILE DIDI LA AZIZ KI KUTUA JANGWANI LIKO HIVI AISEE….YANGA WATEMA ZAIDI YA MILIONI 200…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply