Home Habari za michezo NABI AIPUUZA SIMBA….AKACHA MAANDALIZI YA DABI…ARINGIA UBORA WA KIKOSI…

NABI AIPUUZA SIMBA….AKACHA MAANDALIZI YA DABI…ARINGIA UBORA WA KIKOSI…


Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia Nabi amesema hawana kipya sana cha kujiandaa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba kwani maandalizi yalishafanyika katika mechi 20 walizocheza. “Tumekuwa katika ubora katika mechi zote 20 tulizocheza. Tulipoanza msimu tulikuwa na maandalizi bora kwa kila timu tutakayokutana nayo ikiwemo Simba,” alisema Nabi ambaye.

“Ili uwe bingwa hutakiwi kujiandaa kwa akili ya kukutana na Simba pekee, utashinda mechi mbili za Simba na ukapoteza zingine utashuka daraja, tumekuwa tukijiandaa kiubora kushinda dhidi ya timu yoyote tutakayokutana nayo kwenye ligi.

Aidha Nabi alisema Yanga wanaiheshimu Simba hasa mechi hiyo kwa ubora wao na kikosi chake kitaandaliwa kwa ugumu wa mchezo huo ili wazidi kukimbilia kukamilisha malengo yao.

Alisema wanajua kila kitu juu ya ubora wa Simba iliyo chini ya kocha Pablo Franco na anajua wekundu hao watakuja na nguvu ya kutaka kuwazuia katika kasi yao waliyonayo msimu huu.

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu, hii ni mechi inayobeba presha ya nchi, tunaiheshimu Simba lakini hata wao wanajua ubora wetu, naamini watakuja na akili ya kutaka kutupunguza kasi yetu ugumu wa mchezo utakuwa hapo.”

Kocha huyo ambaye amechukua tuzo mbili za kocha bora kwa miezi miwili tofauti aliongeza hata kama ikitokea hatokuwepo anamuamini msaidizi wake Cedric Kaze ni kocha aliye na ubora wa kusimamia dakika 90 za mchezo huo kwa kuwa alishafanya kabla.

“Hakuna tatizo katika kukosekana kwangu, kama itakuwa hivyo, nimekwambia maandalizi ya msingi yanakuwa yameshafanyika kitu muhimu ni kusimama pale wakati wa mchezo. Namuamini sana Kaze ni mtu bora.‘’ ambaye anastahili kusimama na kuongoza timu, alishawahi kabla na timu ikashinda.

“Kitu bora zaidi kwetu idadi ya majeruhi imekuwa ikipungua sana na sasa tulibaki na watu wawili tu ambao hawakuwa sawa Saido (Said Ntibazonkiza) na Yacouba (Songne) ambaye bado atakuwa nje kwa muda zaidi lakini Saido naamini anaweza kuimarika.

SOMA NA HII  HAJI MANARA ARUDI YANGA NA KAULI YA KUMKATAA ALI KAMWE.