Klabu ya soka ya Yanga hii leo imetimiza mwaka mmoja bila ya kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara .
Nyota wa Yanga Bakari Mwamnyeto(wa kwanza kulia),Dickson Job(katikati) na Kibwana Shomari(kushoto) wakishangilia ushindi
Kwa mara ya mwisho Yanga kufungwa katika michuano ya Ligi Kuu ilikuwa ni April 25,2021 waliponyukwa bao 1-0 na Azam Fc lililowekwa kimiani na mshambuliaji Prince Dube ikiwa ni katika msimu wa 2020/21.
Hicho ndicho kilikuwa kipigo cha kwanza na pekee hadi sasa kwa Kocha wa Klabu hiyo, Mohamed Nabi ambaye alikuwa akiiongoza Yanga kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na miamba hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.
Tangu April 25,2021Yanga imecheza mechi 27 za Ligi Kuu bila kupoteza, imeshinda mechi 21, sare 6 na kwa ujumla msimu huu wanaongoza Ligi wakiwa na alama 54 wakiwa wamecheza mechi 20,wakishinda 17 na kutoka sare tatu.