Habari za michezo

CHELSEA WAKUBALI YAISHE KWA RUDIGER….SASA RASMI KUTAMBULISHWA MADRID MSIMU UJAO…

admin April 26, 2022 1:19 pm


Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel amethibitisha kuwa beki wa kikosi cha timu hiyo, Antonio Rudiger ataondoka kikosini hapo ifikapo mwisho wa msimu huu.

Klabu ya Real Madrid inapewa chapuo la kuinasa saini ya nyota huyo ambaye ana uwezo mkubwa kwenye suala a kutimiza majukumu yake awapo uwanjani.

Nyota huyo anatajwa kuondoka bure kwa kuwa dili lake litakuwa limeisha hivyo anakwenda kupata changamoto mpya kwenye timu nyingine ambayo atahamia.

Inaelezwa kuwa beki huyo yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na Real Madrid na mpaka sasa wamefikia hatua nzuri kwa ajili ya kuinasa saini yake.

Ni mkwaja wa pauni 10.1 milioni ameombwa kulipwa kama mshahara wake kwenye timu hiyo ambayo inatarajiwa kumpa mkataba wa miaka minne.

BAADA YA KUTUA TZ….KAPOMBE AWAWASHIA MOTO YANGA….”MAONGEZI HAYATAKIWI….TUKUTANE April 30…” GEITA GOLD WAO NI MWENDO WA ‘KIMYA KIMYA MZEE BABA’…’WAICHIMBA BITI LA KUFA MTU’ AZAM FC…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply