Home Habari za michezo UKWELI LAZIMA USEMWE…GOLI LA ORLANDO HALIKUWA HALALI…JE..VAR HAINA MSAADA KWA WAAMUZI..?

UKWELI LAZIMA USEMWE…GOLI LA ORLANDO HALIKUWA HALALI…JE..VAR HAINA MSAADA KWA WAAMUZI..?


KOCHA wa mpito wa Manchester United, Ralf Rangnick amehoji uhalali wa matukio manne ambayo VAR ilitolea uamuzi katika mchezo wao dhidi ya Arsenal wa Ligi Kuu England.

Katika mchezo huo, Arsenal ilishinda kwa mabao 3-1 ambayo yalifungwa na Nuno Tavares, Bukayo Saka ambaye alifunga kwa penalti na Granit Xhaka. Bao la Machester United ambayo ilikuwa ugenini lilifungwa na Cristiano Ronaldo.

Moja ya tukio la utata ni lile la Man United kunyimwa penalti baada ya mchezaji wa Arsenal, Cedric Soares kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari wakati Arsenal wakiongoza kwa bao 1-0 na kunyimwa bao lililofungwa na Ronaldo wakati wapinzani wao wakiwa mbele kwa mabao 2-1.

Rangnick alisema mstari uliowekwa wa kuzidi haukuwa sahihi kumnyima bao Ronaldo kuwa alikuwa amezidi. Rangnick pia alisema mshambuliaji wa Arsenal, Eddie Nketiah alizidi wakati akiwa uso kwa uso na kipa David de Gea wakati Xhaka amefunga katika dakika ya 70.

“Mchezaji wa Arsenal aliunawa mpira kipindi cha kwanza na Jadon Sancho alihusika katika tukio hilo,” alisema Rangnick.

“Bao la pili la Ronaldo lilikuwa halali tofauti na uamuzi wa VAR kuwa alikuwa amezidi. Mfungaji alikuwa kwenye mstari mmoja. Nimejiridhisha mara baada ya kuangalia upya mara baada ya mchezo. Unaweza kupitia kwa njia ya picha za marejeo.”

“Bao la tatu la Arsenal halikuwa halali kwani Nketiah alikuwa katikati ya De Gea na Xhaka na pamoja na VAR kurejea na kugundua hivyo, lakini bado ‘waliwapa’ bao Arsenal,” alisema Rangnick.

“Anthony Elanga alikuwa sambamba na Tavares, mchezaji mwingine walikuwa naye. Angalau vilevile kuna hoja. Kilichotea kilikuwa wazi na uwepo wa VAR na waamuzi ni kutoa uamuzi sahihi.”

Aliendelea kulalama kuwa hawakuwa na bahati katika matukio hayo, lakini waliendelea kucheza vizuri na kushambulia.

Orlando Pirates vs Simba

Mashabiki wa mpira wa miguu wapo katika mabishano kuhusiana na bao la mshambuliaji wa Orlando Pirates kutoka Ghana, Kwame Peprah ambalo liliipeleka mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF KESHO....UNAAMBIWA NABI HUKO YANGA HATAKI MZAHA...APANIA KUUA 'SISIMIZI KWA RUNGU'....

Bao hilo liliufanya mchezo huo kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti ambapo Simba ilitolewa rasmi katika mashindano hayo.