Habari za michezo

HUU HAPA UKWELI WA SABABU YA NTIBAZONKIZA KUCHELEWA KUINGIA UWANJANI NA WENZAKE…

admin April 30, 2022 5:36 pm


MSHAMBULIAJI Saido Ntibazonkiza wa Yanga hakuwepo kabisa katika mstari wa wachezaji wenzake wakati wanasalimiana kabla ya mchezo dhidi ya Simba kuanza.

Wakati wachezaji wote wanaingia uwanjani na kwenda kujipanga ili mpira uanze, Ntibazonkiza yeye alichelewa kabisa kuingia uwanjani na walipokuwa wanasalimiana yeye alitoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kwenda kwenye benchi la Yanga.

Wenzake waliposalimiana na kwenda kujipanga kwa ajili ya picha ya pamoja mchezaji huyo bado alikuwa pembeni kwenye benchi.

Mpira ulipowekwa kati Ntibazonkiza aliingia ndani haraka na kwenda kucheza sambamba na wenzake akitokea upande wa kushoto.

Ntibazonkiza alipoingia uwanjani hakuonyesha kuwa na majeraha ambayo yalimfanya akose kusalimiana na wenzake pamoja na picha ya ukumbusho.

KISA ‘KAZI CHAFU’ ZA KIBWANA SHOMARY….MORRISON AJIKUTA AKIZOMEWA UWANJA MZIMA… HAMTUWEZI….INONGA NA MAYELE NI ZAIDI YA BALAA….AUCHO AMTIA CHAMA MFUKONI KAMA NOTI YA BUKU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply