Habari za michezo

KISA ‘KAZI CHAFU’ ZA KIBWANA SHOMARY….MORRISON AJIKUTA AKIZOMEWA UWANJA MZIMA…

admin April 30, 2022 5:27 pm


MSHAMBULIAJI wa Simba, Bernard Morisson amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na mashabiki wa Yanga katika mchezo wao dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kuzomewa kwa Morrison ni baada ya kocha wa Simba, Pablo Franco kumtoa dakika 54 na nafasi yake akiingia Kibu Denis wakati huo huo Sadio Kanoute alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Mzamiru Yassin.

Muamuzi msaidizi wa nne Elly Sasii aliponyanyua kibao cha kubadilisha wachezaji ilipoonekana namba ya Morrison mashabiki wa Yanga walianza kumzomea.

Mchezaji huyo hakuonyesha kujali kwani alitoka bila kuwa na presha yoyote huku akiwa ameinamisha kichwa chini.

Morrison katika mchezo huo alikuwa na wakati mgumu chini ya Kibwana Shomari na hata alipohama upande kwenda kulia alikutana na mabeki Djuma Shaban na Dickson Job.

BREAKING….WAKALA WA POGBA, IBRAHIMOVICH NA HALAAND, MINO RAIOLA AFARIKI DUNIA… HUU HAPA UKWELI WA SABABU YA NTIBAZONKIZA KUCHELEWA KUINGIA UWANJANI NA WENZAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply