Home Habari za michezo ARTETA: TULIKUWA NA KILA KITU CHA KUSHINDA…TATIZO NI SPIDI TU…

ARTETA: TULIKUWA NA KILA KITU CHA KUSHINDA…TATIZO NI SPIDI TU…


MABAO kutoka kwa Leandro Trossard dk 28 na Enock Mwepu dk 66 yaliweza kutosha kuipa pointi tatu Brighton mbele ya Arsenal.

Ni bao la Martin Odegaard dk 89 Uwanja wa Emirates lilitosha kuwafuta machozi washika bunduki hao wanaonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta.

Arteta amesema kuwa walikuwa wana kila kitu cha kuweza kushinda lakini haikuwa hivyo.

β€œTulikuwa na umiliki mzuri wa mpira na ilikuwa nzuri kwetu tulipata nafasi nyingi lakini hatukuweza kuzitumia,hatukucheza katika spidi sahihi,”.

Arteta ametoka kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Crystal Palace Jumatatu huku kichapo hicho kikiwapotezea matumaini ya kuwa ndani Top 4.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WASAUZI....MORRISON NA WENZIE WAPETA CAF....WAFUTIWA ADHABU...