Home Azam FC AZAM WATINGA KIBABE NUSU FAINAL KOMBE LA SHIRIKISHO…YAWAKUNGU’UTA WABABE WA SIMBA…

AZAM WATINGA KIBABE NUSU FAINAL KOMBE LA SHIRIKISHO…YAWAKUNGU’UTA WABABE WA SIMBA…

Matajiri wa Jiji. Timu ya Azam FC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania mchezo uliopigwa Jumatano Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mabao ya Azam FC yamefungwa na Rodgers Kola dakika ya 24, Ismail Aziz Kader dakika ya 45 na Mudathir Yahya dakika ya 78 na sasa Azam FC watamenyana na Coastal Union ya Tanga iliyoitoa Kagera Sugar.

Timu nyingine iliyotinga Nusu Fainali ni Yanga ambayo imeitoa Geita Gold na itakutana na mshindi wa Robo Fainali ya mwisho baina ya mabingwa watetezi, Simba na Pamba.

SOMA NA HII  A-Z NAMNA BALEKE ALIVYOANZA SIMBA KWA MKWARA WA KUFA MTU....DODOMA WAFUNGWA GOLI 12...