Home Habari za michezo BAADA YA KUTOLEWA KOMBE LA SHIRIKISHO..PABLO AVUNJA UKIMYA SIMBA…ATAJA HATUA ZA KUCHUKUA…

BAADA YA KUTOLEWA KOMBE LA SHIRIKISHO..PABLO AVUNJA UKIMYA SIMBA…ATAJA HATUA ZA KUCHUKUA…


Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Franco Pablo Martin amesema hana budi kusahau yaliyotokea Afrika Kusini, ili kuangalia mchezo unaofuata wa Ligi Kuu Tanzania Bara Dhidi ya Young Africans Jumamosi (April 30).

Kocha Pablo pamoja na Kikosi chake atakua ugenini Jumamosi, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kuikabili Young Africans iliyo na njaa ya Ubingwa msimu huu 2021/22, huku akiwa na mpango wa kuzima rekodi ya Wananchi ya kutopoteza mchezo hadi sasa.

Kocha huyo kutoka nchini Hispania amesema kilichotokea Afrika Kusini katika mchezo dhidi ya Orlando Pirates kimemuumiza kila mmoja anayehusika na Simba SC, kwani halikua kusudia lao kuishia hatua ya Robo Fainali, lakini hana namna ya kulisahau hilo na kuangalia ni vipi atingia kwenye mpambano dhidi ya Young Africans.

Amesema mchezo huo ni mtihani mkubwa kwake na kwa wachezaji wake, lakini tayari ameshaanza kujifua ili kukamilisha lengo la kuushinda mtihani huo, ambao utakwenda kushuhudiwa na Mashabiki wengi wa soka Nchini Tanzania na kwingineko Barani Afrika.

“Ni ngumu kusahau kilichotokea Afrika Kusini, halikua kusudia letu kuishia Robo Fainali katika Michuano ya CAF, lakini matokeo ya Soka yameshaamua, tumetolewa na tunapaswa kuangalia lililo mbele yetu kwa sasa.”

“Tunakabiliwa na mchezo dhidi ya Young Africans, kiufundi ni mtihani mwingine kwangu na kwa wachezaji wangu, lakiki tumeshaanza maandalizi ya kupambana dhidi ya wapinznai wetu na tunaamini mambo yatakua mazuri.”

“Ushindi dhidi ya Young Africans utakua ni furaha kwangu, wachezaji na kila mmoja anayehusika na Simba SC, lakini hilo haliwezi kukamilika kama sisi Benchi la Ufundi na wachezaji ambao ndio wapambanaji tutashindwa kujiandaa na kupanga mikakati sahihi ya kuwafunga wapinzani wetu Jumamosi.” amesema Kocha Pablo

Simba SC inakwenda kukutana na Young Africans huku ikiwa na asilimia kubwa ya kuutema ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu, kufuatia kuachwa kwa alama 13 katika msimamo wa Ligi Kuu hadi sasa, huku timu hiyo ikicheza michezo 19.

SOMA NA HII  YANGA ACHENI KUMKOMOA FEI TOTO...VAENI VAZI LA UZAZI...MWACHENI AONDOKE

Young Africans iliyocheza michezo 20 inaongoza msimamo ikiwa na alama 54, ikifuatiwa na Simba SC yenye alama 41, huku Namungo FC ikiwa nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 29 na Azam FC ipo nafasi ya nne kwa kumiliki alama 28.