Home Habari za michezo KISA JEZI YA ORLANDO…JEMEDARI AMTOLEA “POVU” MANARA…”GSM NA YANGA WAMEONEKANA WAPUUZI…”

KISA JEZI YA ORLANDO…JEMEDARI AMTOLEA “POVU” MANARA…”GSM NA YANGA WAMEONEKANA WAPUUZI…”


Mchambuzi wa Soka Jemedari Said Kazumari amemvaa Msemaji wa Yanga HAJI MANARA Baada ya kuvaa jezi ya Orlando Pirates Kwenye interview yake Ndani ya kipindi Cha Sports Arena Cha Wasafi FM.

Ameandika 👇

“Siongei maneno mengi, lakini naongea maneno yafuatayo. Mwaka 2003 Simba waliwatoa Zamalek 🇪🇬 katika hatua za awali, lakini hakuna mtumishi wa Al Ahly aliyekwenda na jezi ya Simba SC”

“Hata Dunia ipinduke hakuna mtumishi wa Kaizer chiefs angevaa jezi ya Simba SC kisa Orlando Pirates kufungwa na Simba,, Brand zao wangezilinda kwa kadri wawezavyo na ujinga wangewaachia mashabiki”

“Unakwenda kwenye moja ya media kubwa, unafanya promotion ya tukio lako kubwa kwa msimu kisha unafanya makosa makubwa ya kubishara ….”

“Unavaa jezi ya Orlando Pirates yenye udhamini wa Vodacom, unamnyima Sportspesa haki yake kwenye jezi ya Yanga na tena analipia ambaye wewe ni mtumishi”

“Unavaa jezi ya Orlando Pirates ambaye Kit supplier wake ni ADIDAS, unamnyima haki (GSM) ambaye ndiye msambazaji wa jezi”

“Haya ni matusi makubwa ya kubishara katika soka la Tanzania. GSM anawekeza Mamilioni ya pesa kuisaidia Yanga ili yeye apate mrejesho wa brand yake lakini Silaha yao muhimu inaitukana brand yao”

“Yanga wakitamani kutangaza jezi yao ili mashabiki wasio na jezi wanunue, msemaji wao anavaa jezi kutoka Africa kusini”

“😭😭 Kwa mara ya kwanza nimeandika kitu huku NALIA, nalia kwa sababu taifa limekosa watu katika maeneo muhimu, wanaoweka pesa kwenye soka wanadharauliwa kiasi hiki?”

“Sportspesa, GSM na mashabiki wote wa Yanga wameonekana wapuuzi mbele ya mtu waliyemuamini”

“NB; Siwachukii nawasaidia mpate thamani au mtengeneze thamani” Jemedari Said mchambuzi akinukuu Kutoka Mangasin Scandal

SOMA NA HII  ILE ISHU YA SHAFIH DAUDA KUFUNGIWA NA TFF KUMBE IKO HIVI AISEE...MWENYEWE AKANA KUHUSIKA...