Home Habari za michezo NAPE MGENI RASMI KESHO SIMBA vs USGN…’VITOCHI’ VYAPIGWA MARUFUKU KWA MKAPA…

NAPE MGENI RASMI KESHO SIMBA vs USGN…’VITOCHI’ VYAPIGWA MARUFUKU KWA MKAPA…


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ,Nape Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika baina ya Simba SC dhidi ya Us Gendermarie utakaochezwa kesho Jumapili ya April 03, 2022 majira ya saa nne kamili usiku kwenye dimba la Mkapa.

Hayo yamebainishwa leo na meneja habari na mawasiliano wa klabu ya Simba , Ahmed Ally alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuelekea maandalizi ya mwisho wa mchezo kuhitimisha  kundi D na kusakata tiketi ya kuelekea hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

“kwenye mchezo wetu wa kesho mgeni rasmi atakuwa ni mheshimiwa Nape Nnauye ambaye ni waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia ya habari na amekubali na kufurahia sanaa”amesema Ahmed Ally

Pia meneja huyo wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba amepiga marufuku mashabiki wenye mawazo ya kununua vitochi na kwenda kuwamulikia wachezaji wa timu pinzani kuacha mara moja kuhusu mpango huo kwani sio utamaduni wa klabu hiyo 

“mliokuwa na mpango wa kununua vitochi au vitu vyenye mwanga achaneni navyo sisi makelele yetu ndio silaha yetu ya kushinda mchezo wa kesho” amesema Ahmed Ally

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO...WACHEZAJI NA MSHABIKI SIMBA WARUHUSIWA "KUMWAGILI MWOYO MAJI"...