Home Habar za Usajili Simba SIMBA WAAMUUA KUKISUKA UPYA KIKOSI CHAKE…WATENGA MAMILION KWA BEKI TU…IBENGE ATIA NENO….

SIMBA WAAMUUA KUKISUKA UPYA KIKOSI CHAKE…WATENGA MAMILION KWA BEKI TU…IBENGE ATIA NENO….


SIMBA inafanya mambo yake kimyakimya. Wameanza mikakati mizito ya kusuka kikosi kipya cha msimu ujao kwa kuangalia eneo moja baada ya jingine.

Na katika kutekeleza hilo, imebainika kwamba wametoa kazi maalum kwa wataalam kuhakikisha wanapata mafundi kwenye maeneo hayo ndani ya muda na bila papara. Wameanza na beki.

Chanzo cha uhakika ndani ya Simba kimeeleza kuwa viongozi wametoa kazi kwa mmoja wa mawakala maarufu anayefanya kazi kwa karibu na wachezaji wa Morocco na DR Congo ili awapatie jembe lingine kali kama Henock Inonga anayeupiga mwingi kwasasa.

 Tathimini ya kiufundi ambayo imekabidhiwa na makocha kwa uongozi ni kwamba mabeki watatu tu ndio wenye angalau uhakika wa kusalia Simba msimu ujao ambao ni Henock Inonga, Joash Onyango na Kennedy Juma. Lakini Simba inataka kumwongeza fundi mmoja mpya ambaye atakamilisha pea mbili za mabeki wa kati.

Habari zinasema kwamba Simba wamepania kumaliza kabisa tatizo la krosi, faulo na mipira ya juu linalowasumbua mara kadhaa kwenye mechi za kimataifa ndio maana wamekubaliana kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye nafasi hiyo ya ulinzi.

 Simba inapiga hesabu kimyakimya za kuachana na mkongwe Pascal Wawa  ambaye hivi karibuni amekuwa akikosa nafasi ya kuanza mara kwa mara akizidiwa ubora na Inonga na Onyango ambao wamekuwa wakiwa chaguo la kwanza ingawa bado Kocha Pablo Franco amesisitiza kutaka mbadala wao imara zaidi.

Hata hivyo mkataba wa Onyango ambaye ni Mkenya na Simba unafikia tamati mwisho wa msimu huu na tayari uhakika mabosi wa wekundu hao wameanza kufanya mazungumzo naye ili abaki kwa miaka mingine miwili zaidi ingawa inadaiwa anataka mshahara mnono ambao baadhi ya viongozi wameguna lakini hawajafanya uamuzi wa mwisho.

Mabosi wa Simba wanaona Onyango ameanza kuelewana vizuri na Inonga lakini endapo hawatapata mtu mwingine bora wa kuwapa presha ya nafasi wanaweza kupungua ubora zaidi kutokana na kutopata changamoto mpya sambamba na muda wa kupumzika. Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Salim Abdallah alisema hivi karibuni kwamba wataisuka Simba mpya na inaweza kuwa na sura mpya zisizozidi nne za maana.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUAMRIWA KURUDI YANGA...FEI TOTO AIGOMEA TFF...WAKILI WAKE KAANIKA A-Z....

Kocha wa RS Berkane, Florent Ibenge ambaye ana urafiki na baadhi ya mabosi wa Simba amethibitishia kwamba anafahamu Simba iko sokoni inatafuta beki wa kati na kwenye pitapita zake sokoni mmoja wa mawakala wa Berkane anayefanya kazi hiyo amewadokeza hilo.

“Nadhani wanaona mabeki wao hawaruki vizuri lakini kuna baadhi wanaona hawastahili kuwa nao kwa msimu ujao,mimi sijawajua,”alisema Ibenge ambaye amehusika kwa asilimia kubwa kuleta wachezaji wakubwa wa DR Congo wanaotamba nchini kwa sasa akiwemo Fiston Mayele.

“Unapokuwa na malengo makubwa katika mashindano haya ya Afrika kuna aina ya ubora wa wachezaji unawahitaji,unajua Simba ni timu nzuri ina wachezaji wenye ubora lakini kama wanataka kujisuka zaidi lazima wapate mabeki bora,”aliongeza Ibenge ambaye ni Kocha wa zamani wa AS Vita ambaye mara zote ameshindwa kuifunga Simba kimataifa ndani ya Uwanja wa Mkapa.

Simba imepania kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho msimu huu na wikiendi hii itakipiga na USGN kuwania kufuzu robofainali.