Habari za michezo

WAKATI WADAU WAKIMTILIA SHAKA KUHUSU KIMO CHAKE KAMA BEKI…DICKSON JOB AIBUKA NA KUWAJIBU HAYA…

admin May 5, 2022 2:07 pm


Beki Dickson Job wa Yanga amesema hayupo tayari kuona timu yake inapoteza kwa sasa kwa sababu lengo lao ni kumaliza Ligi bila kufungwa.

Yanga mpaka sasa wamecheza mechi 21 bila kupoteza na kuifanya iwe timu pekee ambayo haijafungwa kwenye Ligi.

Akizungumza Job alisema;

“Kikubwa mpaka sasa kwanza atuhitaji kupoteza mchezo wowote na ili tusipoteze tunahitaji kucheza mechi bila kuruhusu goli kwa kila mchezo, sisi kama walinzi wa timu tupo tayari kwa ajili ya kupambana ili kutimiza malengo yetu.”

Job aliongeza kuwa;

“Mimi na Mwamnyeto tuna maelewano makubwa na kucheza kwetu muda mrefu tunajuana vizuri na ndio maana kila mmoja anatoa kile anachostahili kwa wakati.”

Job amejiunga na Yanga kwenye msimu dirisha dogo la msimu uliopita na tangu ameingia kwenye kikosi cha Nasreddine Nabi amejihakikishia nafasi akicheza sambamba na Bakari Mwamnyeto.

Awali mashabiki wa Yanga walikuwa na wasiwasi na kimo cha Job.

WAKATI TETESI ZA KUWA KWENYE UGOMVI NA CHAMA ZIKIZIDI KUKUA…PABLO AIBUKA NA KUSEMA HILI… BAADA YA NDOTO ZOTE KUBWA ZA SIMBA KUFELI MSIMU HUU…WABADILI GIA ANGANI.. WAOTA UBINGWA WA ASFC..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply