Habari za michezo

IMETOSHAAA….YANGA SARE SASA BASI…KAZE AFUNGUKA KINACHOWATESA…MASHABIKI WAHUSISHWA…

admin May 12, 2022 12:47 am


MARA baada ya kupata suluhu katika michezo mitatu mfululizo kwenye ligi kuu, benchi la ufundi la timu hiyo, limesema kuwa kwa sasa inatosha na litapambana kuhakikisha kuwa timu hiyo inapata ushindi katika michezo inayofuata na kuendeleza matumaini ya ubingwa msimu huu.

Yanga imeshindwa kupata ushindi wala kufunga bao katika michezo mitatu iliyopita mfululizo dhidi ya Simba, Ruvu Shooting na Tanzania Prisons.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze alisema kuwa matokeo ambayo wameyapata katika michezo iliyopita yamewasikitisha na watapambana kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo ujao ili kuendelea na mbio za kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

“Tunatakiwa kuhakikisha tunashinda katika michezo yetu ijayo, matokeo ya michezo iliyopita sio mazuri kwetu na tumeumia kuona tumepata matokeo haya, sio wachezaji wala viongozi wote tumeumia sana.

“Mashabiki pia lazima watakuwa wanaumia na haya matokeo na muhimu kwa sasa ni matayarisho ya michezo ijayo ambapo tunatakiwa kufanya vizuri zaidi kwa kupata ushindi ili kuendelea kuwa karibu na ubingwa,” alisema kocha huyo.

WAARABU WAMFANYIA KUFURU STRAIKA SIMBA SC…SAIDO APEWA MWAKA…YANGA WATENGA BIL 5 ZA UBINGWA TU… RAIS WA FIFA NA MASTAA WA SOKA KUTUA TANZANIA…KARIA AFUNGUKA ‘SHOW’ NZIMA ITAKAVYOKUWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply