Habari za michezo

AS ROMA NA MOURINHO WAWEKA HISTORIA HII MPYA ULAYA…KILA MMOJA KAMNUFAIKA MWENZAKE..YANI NIPE NIKUPE….

admin May 26, 2022 12:39 pm


Jose Mourinho ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza barani ulaya kushinda makombe 3 tofauti ya vilabu barani ulaya baada ya kukiongoza kikosi cha AS Roma kutwaa ubingwa wa michuano ya Europe Conference League jana usiku.

AS Roma chini ya Jose Mourinho wametwaa ubingwa wa Connference na kombe lao la kwanza kwenye michuano ya vilabu Ulaya kwa kuinyuka Feyenoord ya Uholanza kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali, bao pekee la mchezo huo limefungwa na Nicolo Zaniolo dakika ya 32.

Ubingwa huu umemfanya Mourinho kufikisha idadi ya makombe 5 ya vilabu barani ulaya aliyoshinda kama kocha. ameshinda ubingwa wa Klabu Bingwa (Uefa Champions League) mara 2 akiwa na FC Porto mwaka 2004, na Inter Milan 2010, pia ameshinda ubingwa wa Michuano ya UEFA Europa League mara mbili akiwa na FC Porto mwaka 2003 na 2017 akiwa na Manchester United. Hivyo ubingwa wa usiku wa jana ni wa 5 katika michuano 3 tofauti.

Mourinho pia hajapoteza mchezo hata mmoja wa fainali aliocheza kwenye michuano ya vilabu barani Ulaya katika fainali zote 5 alizocheza ameshinda zote. Na kombe hili ni la 26 kwa kocha huyo raia wa Ureno katika miaka yake 19 ya ukocha. 

WAKATI MATANGAZO YAKIWA ‘LIVE’… BBC WAIITA MAN UTD TAKATAKA…CEO WAO AFICHUA ALIYEFANYA MCHEZO HUO… KUHUSU ISHU YA KUTEMANA NA YANGA…NTIBAZONKIZA APANGA KUTAPIKA NYONGO…”SITARUHUSU MTU ANICHAFUE”…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply