Habari za michezo

KAPOMBE, MANULA WASHUSHA PRESHA SIMBA…AHMED ALLY AFUNGUKA ‘MBILINGE KAKARA’ LILIVYO KABLA YA J/MOSI…

admin May 26, 2022 12:19 pm


MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema nyota wawili waliokuwa majeruhi katika kikosi chao, Aishi Manula na Shomari Kapombe, wameanza mazoezi rasmi kujiandaa kuikabili Yanga SC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, Jumamosi hii.

Ally alisema: “Tunaendelea na maandalizi yetu ambapo kwa sasa tunautumia Uwanja wa Gwambina kufanya mazoezi, kiukweli maandalizi yanaendelea vizuri na mkakati wetu ni kuhakiisha tunapata ushindi mbele ya Yanga.

“Habari njema ni kwamba wachezaji wetu wawili ambao ni Shomari Kapombe aliyeumia nyama za paja tulipocheza dhidi ya Geita pamoja na Aishi Manula ambaye alikatwa na vioo kwenye vidole, wanaendelea vizuri na tayari wameanza mazoezi na wenzao, tunaamini kuelekea mchezo ujao watakuwa sehemu ya kikosi kitakachopambana na Yanga.”

KUELEKEA MECHI YA J/MOSI…MO DEWJI KAIBUKA NA HILI SIMBA…KATOA MAAGIZO MAZITO KWA TRY AGAIN NA BARBARA… KISA ISHU YA SAIDO NA AMBUNDO KUSIMAMISHWA…MAYELE, SHABANI DJUMA WAJILIPUA YANGA…’WAMFESI’ NABI BILA UOGA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply