Habari za michezo

A-Z JINSI RAIS SAMIA ‘ALIVYOWAKA WAKA’ NA KOMBE LA DUNIA LEO…AANIKA SABABU ZA FIFA KUICHAGUA TZ…

admin May 31, 2022 4:40 pm


Rais Samia Suluhu Hassan leo Mei 31, 2022 amepokea kombe la Dunia Ikulu jijini Dar es Salaam  ambalo litakaa kwa siku mbili nchini kabla ya kuondoka.

Kombe hilo amekabidhiwa na mchezaji mkongwe wa Brazil Juliano Belletti ambaye anaongoza timu katika ziara ya kombe hilo nchini.

Akipokea kombe hilo Rais Samia amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kesho Juni 1, 2022 kufika Uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam kupiga  picha na kombe hilo.

Tanzania inakua miongoni mwa nchi tisa za Afrika  ambazo imepata bahati ya kupitiwa na kombe hilo.

Samia amefafanua kuwa Tanzania imechaguliwa kuwa miongoni mwa nchi hizo kutokana na kuendelea kufanya vizuri kwenye michezo ambapo amesema watanzania wengi wanapenda soka.

Kesho kombe litaanza kuonyeshwa kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni na baada ya hapo itaonyeshwa filamu ya Royal tour.

Rais ametoa rai kwa watanzania kutumia ujio wa kombe la Dunia nchini kuitangaza  Tanzania duniani.

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amemshukuru Rais kwa kufanya mapinduzi makubwa kwenye michezo katika kipindi kifupi cha utawala wake.

PABLO ALIAMSHA HUKO…AKATAA KUPOKEA BARUA YA KUVUNJA MKATABA…ADAI HAKUPANGA KUONDOKA SIMBA MAPEMA… WAKATI LIVERPOO WAKIMTAKA SON KAMA MBADALA WA MANE….ARSENAL WAJICHOMOZA KUTIKISA KIBERITI….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply