Habari za michezo

PABLO ALIAMSHA HUKO…AKATAA KUPOKEA BARUA YA KUVUNJA MKATABA…ADAI HAKUPANGA KUONDOKA SIMBA MAPEMA…

admin May 31, 2022 4:32 pm


VIKAO vya siku mbili ndani ya Simba vimeamua rasmi kuachana na kocha mkuu Pablo Franco kwa kile kilichodaiwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.

Simba imepoteza mataji yake yote mawili la Ligi Kuu Bara ambalo walilitwaa kwa mara nne mfululizo pamoja na taji la Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) walilobeba mara mbili mfululizo.

Habari za kikao hicho zilisema kwamba wamefikia makubaliano hayo na tayari Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alimwandikia barua ya kuvunja mkataba kocha huyo aliyomtumia jana jioni.

Pablo amekiri kupokea barua hiyo na kwamba alimrudishia bosi wake kwani kuna vitu ndani ya barua hiyo vilikuwa havijakaa sawa hivyo anachosubiri sasa ni Barbara kufanya marekebisho hayo ili asaini.

“Ni kweli tulikuwa na kikao na mabosi wangu na kuna mambo sikukubaliana nayo hususani upande wa usajili, jioni CEO alinitumia barua ya kuvunja mkataba lakini ilikuwa na upungufu hivyo sikusaini nilimrudishia ili arekebishe.

“Sikupanga kuondoka Simba kwani tayari nilikuwa nimeikatia Visa familia yangu ya kuishi hapa kwa mwaka mmoja, hivyo nasubiri akirekebisha hiyo barua na kuyaweka yale niliyoyapendekeza ambayo ni maslahi basi nitasaini kuvunja mkataba,” amesema Pablo ambaye aliingia Simba Novemba mwaka jana.

BAADA YA NTIBAZONKIZA ‘KUSEPESHWA’ YANGA…MAYELE AFICHUA MENGINE YA SIRI BAINA YAO WAWILI… A-Z JINSI RAIS SAMIA ‘ALIVYOWAKA WAKA’ NA KOMBE LA DUNIA LEO…AANIKA SABABU ZA FIFA KUICHAGUA TZ…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply