Habari za michezo

BAADA YA ‘KUFANIKIWA KUMZUIA MAYELE JUZI’…. SIMBA KUKUTANA NA ‘CHUMA CHA PUA’ LUSAJO….

admin May 2, 2022 7:44 am


Klabu ya soka ya Simba imetua rasmi mkoani Mtwara tayari kuwakabili Namungo FC katika pambano la Ligi Kuu ya NBC kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Mei 3 2022 katika Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

Simba inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao moja bila kwenye mchezo wa awali ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam bao lililofungwa na mshambuliaji Meddie Kagere dakika za majeruhi.

Kwa mujibu wa msimamo wa Ligi Simba ipo katika nafasi ya pili ikiwa na jumla ya alama 42 alama 13 nyuma ya vinara Yanga ambao wana jumla ya alama 55 lakini Simba ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Mchezo wa kesho ni muhimu kwa timu zote mbili kwani Namungo FC ikipoteza mchezo huo kimahesabu itakuwa tayari imejitoa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu huku Simba nayo inalazimika kushinda ili kufufua matumaini ya kutetea ubingwa wake.

BAADA YA KUISHINDWA SIMBA JUZI….YANGA WAPAA KWA HASIRA ZOTE KWENDA KIGOMA… RASMI…SIMBA WAUKATIA TAMAA UBINGWA LIGI KUU…AHMED ALLY ‘KINYOONGEEEH’ KAFUNGUKA HAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply