Home Habari za michezo BAADA YA KUONGEZA MKATABA YANGA…KIBWANA AFUNGUKA MAZITO…ADAI KUNA WASIOMPENDA…

BAADA YA KUONGEZA MKATABA YANGA…KIBWANA AFUNGUKA MAZITO…ADAI KUNA WASIOMPENDA…


Beki wa Yanga Kibwana Shomari, amesema kuwa anafurahia kuwa ndani ya kikosi cha Yanga na ana imani ya kuendelea kufanya vizuri baada ya kuongeza mkataba wa miaka miwili.

Kibwana Shomari amesaini mkataba wa miaka mwili kuendelea kuitumikia timu ya wananchi Yanga.

Mkataba wa beki huyo chaguo la kwanza la Kocha Nasreddine Nabi ulikuwa unakaribia kufika ukingoni mwa msimu huu hivyo bado yupo sana ndani ya kikosi cha Yanga.

”Nipo ndani ya Yanga kwa sasa na hii ni habari nzuri kwa wengi ambao wanapenda mimi kuwa hapa kwa Wananchi kuendelea kufanya kazi”Kibwana amesema:”

“Kwa wale ambao hawapendi nina amini kwamba itawauma basi wakae kimya na kwa sasa nipo ndani ya Yanga kama Wananchi wamenitaka mimi nani niweze kukataa kusaini Yanga?”Kibwana amesema:”

Mei 10 Yanga walitoa taarifa rasmi kuhusu nyota huyo kuongeza mkataba wa miaka miwili kuweza kuendelea kuitumikia timu hiyo.

SOMA NA HII  MBRAZIL SIMBA ASEMA HANA PRESHA...YANGA YATAMBA KULIPA KISASI