Habari za michezo

FT: SIMBA SC 4-0 PAMBA FC….MHILU AONA MWEZI LEO….KIBU MWENDO WA KIMYA…SIMBA WAIFUATA YANGA KIBABE..

admin May 14, 2022 6:15 pm


SIMBA SC wametinga Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Azam Sport Federation (ASFC) na kuifuata Yanga kibabe baada ya kuichapa mabao 4-0 Timu ya Pamba FC kutoka Mwanza Mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na Peter Banda dakika ya 45 kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi ya Rally Bwalya bao lililopelekea Simba kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza bao moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko huku Simba ikinufaika zaidi na mabadiliko hayo.

Kibu Denis aliwanyanyua mashabiki wa Simba dakika ya 47 akifunga bao mara baada ya kupokea krosi ya Mohamed Hussein na mabaao mawili yamefungwa na Yusuph Mhilu dakika ya 52 na 88.

Kwa ushindi huo Simba watakutana na Yanga Nusu Fainali ya Michuano hiyo huku Azam FC watakutana na Coastal Union.

KUELEKEA MECHI YA KESHO DHIDI YA DODOMA….YANGA WAPATA PIGO…. YANICK BANGALA NAYE ‘OUT’… MORRISON AIBUA MAPYA SIMBA…ABEBA KILA KITU KAMBINI…AZIZI KI AJIPELEKA MSIMBAZI…MOSES PHIRI KUTUA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply