Home Habari za michezo KICHUYA AJISOGEZA SIMBA NA YANGA KIULAINIIII…ATUPIA MIGOLI YA KIDEO TUPU NAMUNGO WAKITAKATA...

KICHUYA AJISOGEZA SIMBA NA YANGA KIULAINIIII…ATUPIA MIGOLI YA KIDEO TUPU NAMUNGO WAKITAKATA LEO….


WAKATI shangwe la pointi tatu za mezani na mabao matatu iliyozawadiwa mchana na kamati ya saa 72 halijaisha, Namungo imevuna ushindi mwingine ugenini dhidi ya Biashara United.

Namungo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ambao umechezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza saa 10 jioni.

Mfalme wa shoo hiyo ni Shiza Kichuya aliyeipachika mabao yote mawili akiipatia timu yake pointi tatumuhimu ambazo zinaipeleka timu hiyo kwenye nafasi ya tatu kutoka ya sita baada ya kufikisha pointi 36.

Kichuya ambaye taarifa zinasema kuwa anawindwa na klabu za Simba na Yanga, huku Simba wakiwana shauku kubwa ya kumrudisha nyumbani, amefunga mabao hayo katika dakika ya 9 kwa shuti kali kwa mguu wa kulia akiunganisha krosi ya Reliant Lusajo aliyepokea pande safi kutoka kwa Abdulaziz Makame.

Bao la pili lilipachikwa mnamo dakika ya 66 na Kichuya kwa mguu wa kushoto akifanya juhudi binafsi na kuwachambua mabeki kisha kufumua shuti lilojaa wavuni na kumwacha mlinda mlango wa Biashara United, Daniel Mgore amesimama na asijue la kufanya.

Dakika 10 za mwisho Biashara United iliamka usingizini ikilishambulia kwa nguvu lango la Namungo na hatimaye ikapata bao la kusawazisha katika dakika ya 85 kwa mkwaju wa frikiki uliopigwa na Ambrose Awiyo.

Licha ya kupoteza mchezo huo Biashara United ilicheza vyema na kutengeneza nafasi nyingi ambazo zilishindwa kutumiwa vyema na washambuliaji wake wakiongozwa na Collins Opare.

Ushindi wa leo unaipeleka Namungo kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi baada ya kufikisha pointi 36 huku Biashara United ikisalia kwenye nafasi ya 14 na alama zao 23.

Kocha wa Biashara United, Vivier Bahati amesema uwanja siyo tatizo kwa timu yao kutopata matokeo katika michezo miwili ya nyumbani waliyocheza jijini Mwanza huku akiwataka mashabiki kuwa wavumilivu kwani wanapambana kuiokoa timu hiyo.

SOMA NA HII  BANGALA NA DODOMA JIJI SASA MAMBO NI MUSWANO....KUANZA KUVAA JEZI YAO RASMI...