Home Habari za michezo KIMENUKA YANGA HUKOO…NABI ‘ACHENJIWA’ KISA SURE BOY….MWENYEWE ADAI FEI TOTO NI BORA...

KIMENUKA YANGA HUKOO…NABI ‘ACHENJIWA’ KISA SURE BOY….MWENYEWE ADAI FEI TOTO NI BORA KWAKE…

 


BAADA ya mashabiki wa Yanga kuja juu kupinga mabadiliko ya kumtoa Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ na kuingia Heritier Makambo, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mtunisia Nasreddine Nabi ameibuka na kutaja sababu ya kumtoa nyota huyo.

Tukio hilo la aina yake lilitokea mara baada ya Nabi kufanya mabadiliko hayo akitafuta ushindi wakati timu yake ilipovaana dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa juzi Jumatatu, mechi ambayo iliisha suluhu.

Mabadiliko hayo yalisababisha fujo majukwaani kwa kile kilichoonekana kuchukizwa na mabadiliko hayo ambayo wenyewe walitaka kiungo Said Ntibazonkiza ‘Saido’ ndiye aliyetakiwa kutolewa na siyo Sure Boy.

Akizungumzia hilo, Nabi alisema kuwa sababu ya kumtoa Sure Boy ni kupunguza kiungo mmoja na badala yake kumuongeza mshambuliaji kwa lengo la kupata ushindi katika mchezo huo.

Nabi alisema kuwa alimbakisha Feisal Salum ‘Fei Toto’ kutokanana uwezo wake mkubwa wa kukaba ambao amemzidi Sure Boy mara baada ya kuongeza idadi ya washambuliaji.

Alisema kuwa kama Sure Boy angekuwa ana uwezo mkubwa kukaba, basi asingemtoa na badala yake angeendelea kumbakisha kupambana uwanjani.

“Nisifikiriwe vibaya na mashabiki wa Yanga, nimewaona na kuwasikia mashabiki wakichukizwa na mabadiliko ambayo nimeyafanya ya kumtoa Sure Boy.

“Nilifanya mabadiliko hayo ya kiufundi yenye faida baada ya kuona mshambuliaji mmoja akishindwa kupambana na wachezaji wa Prisons ambao walikuwa wengi golini kwao.

“Kutokana na uhitaji wa washambuliaji, nikaona nimtoe Sure Boy na kumbakisha Fei Toto ambaye ni mzuri katika kuzuia mashambulizi na kumuingiza Makambo.

“Fei Toto ni mzuri katika kukaba katika safu ya kiungo ambaye yeye anaanzia juu, tofauti na Sure Boy ambaye siyo mzuri katika kukaba,”alisema Nabi.

SOMA NA HII  AMBUNDO: WALIMU AMEKUWA AKITUSISITIZA TUFANYE KAZI KWA JUHUDI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here