Home Habari za michezo KISA MAYELE KUKOSA PENATI JUZI…NABI NAYE KAONA LISIMPITE HIVI HIVI…AIBUKA NA HILI...

KISA MAYELE KUKOSA PENATI JUZI…NABI NAYE KAONA LISIMPITE HIVI HIVI…AIBUKA NA HILI JIPYA…


BAADA ya kushuhudia timu yake ikitoka sare ya tatu mfululizo juzi huku akimtetea Fiston Mayele kwa kukosa penalti, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema katika mbio za ubingwa hawatakiwi kuangalia mpinzani wao bali wanaelekeza nguvu katika kupambana tu.

Nabi aliyasema hayo juzi usiku baada ya kukamilika kwa dakika 90 dhidi ya Prisons na timu hizo kutoka suluhu katika mchezo huo wa Ligi Kuu uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Nabi alisema matokeo yao dhidi ya Tanzania Prisons hayakuwa mazuri kutokana na kupoteza pointi mbili kuelekea mbio za ubingwa na sasa anaangalia namna ya kuweka mambo sawa timu kufanya vizuri katika michezo iliyopo mbele yao.

Alisema kuhusu tofauti ya pointi 11 na aliyekuwa chini yake (Simba), kwenye mbio za ubingwa hawezi kumfikiria mpinzani wake, kwani anachotakiwa kuangalia yeye na wachezaji wake ni mapungufu ya kikosi chako ikiwa ni pamoja na mashabiki kushirikiana kurejesha morali kwa wachezaji ili kuendelea na mapambano.

“Suala la ubingwa siwezi kulizungumzia kwa sababu ninachoangalia ni nini nifanye ili kurudisha morali ya wachezaji wangu kwa lengo la kwenda kutafuta matokeo mazuri katika michezo iliyopo mbele yetu,” alisema Nabi.

Kuhusu Mayele, Nabi alisema:“Hakulazimisha kupiga penalti ili awe mfungaji bora bali alipiga kwa ajili ya kutafuta ushindi, mechi ilikuwa na ushindani na wachezaji walipambana, lakini matokeo si mazuri.”

Alisema mbali na kukosa penalti hiyo pia walitengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia na kwamba hilo ameliona na wanarejea mazoezini kufanyia kazi kwa ajili ya michezo ijayo.

SOMA NA HII  A-Z NAMNA BALEKE ALIVYOANZA SIMBA KWA MKWARA WA KUFA MTU....DODOMA WAFUNGWA GOLI 12...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here