Home Habari za michezo KISA YANGA…BARBARA AITWA KUHOJIWA TFF…ATUHUMIWA KUTOA SHUTUMA ZA UONGO…MANARA NAYE ATAJWA…

KISA YANGA…BARBARA AITWA KUHOJIWA TFF…ATUHUMIWA KUTOA SHUTUMA ZA UONGO…MANARA NAYE ATAJWA…


OFISA Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez atafikishwa mbele ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutoa ushahidi wa shutuma anazodaiwa kuzitoa wakati akihojiwa na na Kituo cha Radio cha METRO FM nchini Afrika Kusini hivi karibuni.

Katika taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa, Klabu ya Yanga iliwasilisha malalamiko yao kwa TFF dhidi ya Barbra ikidai kuwa ali Barbara akihojiwa na radio hiyo alitoa shutuma zisizo za kweli dhidi ya Yanga.

Pamoja na mambo mengine, inadaiwa kuwa, Barbara alitoa kauli ya kulidharirisha Taifa katika masuala ya soka na kusema kwamba; “Tanzania tuna ushindani mkubwa, wakati mwingine vitu vinatumika kuharibu taswira nzuri ya Simba.”

Barbara amethibitisha Kuwa amepokea barua ya kuitwa na Kamati ya Maadili ya TFF hapo kesho, Jumamosi, Mei 21, 2022, saa 4:00 asubuhi kwenye Ofisi za Shirikisho hilo huku akisema hajaelezwa sababu ya kuitwa hapo na ataenda na kuongeza kwamba atakwenda na mwanasheria wake.

“Hata sijui kuna kitu gani, lakini nimepokea barua ya kuitwa na Kamati ya Maadili. Saa 4 asubuhi natakiwa niwe nimeshafika. Nilitegemea nitapata ufafanuzi wa nilichoitiwa, lakini sijaona hicho kitu. Nitaenda na nitakuwa na Mwanasheria wang,” amesema Barbara.

Awali TFF walikanusha kukaa kikao cha maadili kumjadili Barbara lakini leo taarifa imetoka rasmi kuwa Barbara ameitwa kwenye kikao cha maadili TFF. Kwa upande mwingine, Klabu ya Simba inamlalamikia Msemaji wa Yanga, Haji Manara alitoa shutuma zisizo za kweli dhidi ya klabu hiyo, hivyo mashauri yote mawili yatasikilizwa kesho.

SOMA NA HII  KISA JANJA JANJA YA MAYELE NA WENZAKE...PABLO AFANYA KIKAO KIZITO NA INONGA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here