Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA LEO HAPO BAADAYE..YANGA WAINGIA KITETE CHA KUPATA SARE ...

KUELEKEA MECHI YA LEO HAPO BAADAYE..YANGA WAINGIA KITETE CHA KUPATA SARE NYINGINE TENA…


YANGA itashuka uwanjani leo, huku ikiwa haijaonja ushindi katika mechi mbili zilizopita, lakini Kocha Msaidizi, Cedric Kaze amesema sare imewapa kazi ya kupambana zaidi.

Kaze alisema matokeo yaliyopita hayakuwaridhisha, lakini yamewapa nguvu na hamasa kwa michezo ijayo.

“Kila shabiki anapenda kuona tukishinda kila mchezo ingawa huwezi kuacha kuwapa sifa wapinzani wetu ambao nao kwa kiasi kikubwa walicheza vizuri na kuonyesha upinzani kwetu,” alisema.

Kuhusu mabadiliko ya kikosi ambayo mara kadhaa yamekuwa ya kikosolewa na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo, Kaze alisema ana heshimu mitazamo ya watu ila mchezaji anacheza kutokana na jitihada zake katika uwanja wa mazoezi.

Kaze alikiongoza kikosi hicho kutokana na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kufungiwa michezo mitatu kwa madai ya kutoa maneno makali dhidi ya waamuzi wa mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Geita Gold.

Michezo mitatu ambayo Kaze ameiongoza timu hiyo ameshinda mmoja tu dhidi ya Namungo mabao 2-1, April 23, ila baada ya hapo ameambulia suluhu ya 0-0, katika mechi mbili za Simba April 30 na Ruvu Shooting Mei 4.

Yanga inakabiliwa na kibarua kingine leo wakati itakapocheza na Maafande wa Tanzania Prisons katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam huku ikiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, katika mchezo wa kwanza uliopigwa Desemba 19, 2021.

SOMA NA HII  VIDEO: WACHEZAJI BONGO WAAMBIWA WASIPOTELEE KWENYE BANGI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here