Habari za michezo

MBALI NA MORRISON …HAWA HAPA WACHEZAJI WENGINE WATATU WATAKAO KOSEKANA SIMBA…..

admin May 14, 2022 9:57 am


Simba SC wanakipiga na Pamba FC katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Katika mchezo huo itawakosa Clatous Chama, Sadio Kanoute, Taddeo Lwanga ambao ni majeruhi pamoja na Bernard Morrison ambaye ameagwa na timu hiyo.

Simba itakuwa ikisaka taji la tatu mfululizo la mashindano hayo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita na ule wa 2019/2020 na kihistoria ndio timu iliyotwaa ubingwa wa mashindano hayo mara nyingi tangu yaliporudishwa upya msimu wa 2015/2016.

Na endapo itaibuka na ushindi dhidi ya Pamba leo hii, itakutana na Yanga SC kwenye mechi ya nusu fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa katika soka la bongo.

ISHU YA MORRISON KAMA MUVI VILEEE…PABLO AMTIMUA FASTA KAMBINI…MIDOLA YA GSM YATAJWA… MCHEZAJI SIMBA ‘AMSAGIA KUNGUNI’ MORRISON…AWAAMBIA YANGA WASITHUBUTU KUMSAJILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply