Habari za michezo

MKATABA MPYA WA KIBWANA NA YANGA NI ZAIDI YA KUFRU…KULIPWA MAMILIONI YA PESA KAMA ULAYA…

admin May 11, 2022 2:30 am


BEKI wa Kulia wa Klabu ya Yanga Kibwana Shomari amesaini mkataba wa miaka mwili kuendelea kuitumikia timu ya wananchi Yanga.

Mkataba wa Kibwana ulikuwa unamalizika mwisho wa msimu huu, hivyo kwa mkataba huo ataendelea kuwatumikia wananchi kwa miaka mingine miwili mbele.

Taarifa za kuongezwa kwa kandarasi ya Kibwana Shomari zimethibitishwa na Klabu ya Yanga kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Inadaiwa kuwa, mkataba huo unamfanya Kibwana kuwa miongoni mwa mastaa wa Yanga wanaolipwa mkwanja wa maana kwa sasa klabuni hapo.

Chanzo cheti ndani ya Yanga, kinaeleza kuwa, Kibwana pamoja na posho, bonasi za mechi pia atakuwa akikunja kibindoni mshahara wa kati ya Milioni 3.5 mpaka 5, kiwango ambacho wachezaji wengi wazawa wamekuwa wakilipwa na klabu hiyo.

Hii ni kusema kwamba, kwa miaka yote miliwi, Kiwabana atakomba mshahara wa milioni kati ya 84 mpaka 120, na hiyo ni nnje ya posho za safari, na bonasi ya timu kushinda mechi mbalimbali na ubingwa wa mashindano ambayo Yanga watashiriki.

KISA MAYELE….MASTAA YANGA ‘WAPIGWA BITI’..NABI ‘AFURA’ KWA HASIRA..SIMBA WAMPA MASHARTI PABLO… PAMOJA NA TETESI ZA KUTAKIWA NNJE..ONYANGO ANOGEWA NA UTAMU WA SIMBA…AKUBALI ‘KUSINYA’ UPYA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply